Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbahu aliyekuwa na mpango wa kwenda Sweden kufanya majaribio, Kavumbagu, mambo yake si mazuri.
Hali hiyo inatokana na timu iliyokuwa imemuomba mchezaji huyo raia wa Burundi kuwa kimya.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema kama mambo ya Kavumbagu yataendelea kuwa kimya, atabaki klabuni hapo kushiriki msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine ambayo timu hiyo inashiriki.
"Ile timu wamekaa kimya hadi sasa, kama itaendelea kuwa hivia basi ataendelea na majukumu yake ya kawaida," alisema Hall raia wa Uingereza.
Hata hivyo, bado kocha huyo amekuwa hamtumii Kavumbagu mara kwa mara, hali iliyosababisha aombe kujiunga na Simba kwa mkopo hata hivyo Hall hakukubaliana na hilo.







0 COMMENTS:
Post a Comment