Hisia zisizo sahihi, au hisia za kizamani ni sehemu ya mambo ambayo yamekuwa yakiiangusha michezo nchini.
Mchezo wa soka, ndiyo unaathirika sana na wakati
mwingine wanawake huonekana kama adui.
Lakini nchi zinazopiga hatua kimichezo ukiwemo wa soka
zinakwenda njia tofauti kabisa na Afrika Kusini.
Angalia mwandalala huyo mrembo ambaye ndiyo kiungozi
wa mazoezi ya viungo ya timu ya vijana ya taifa ya Afrika Kusini.
Vijaan chini ya miaka 23, wengi wao wakiwa wanacheza
katika timu za Ligi Kuu na zile za ligi daraja la kwanza. Maana yake wana fedha
na wanalipwa mishahara mikubwa, unaweza kusema wana maisha yao mazuri.
Lakini mazoezi yao ya viungo yanaongozwa na dasa
mrembo kabisa ambaye kama ingekuwa Tanzania, angeonekana ni adui.
Mfano, timu ingepoteza mchezo, gumzo lingekuwa huyo
dada. Lakini kama timu ingecheza vibaya, dada angekuwa gumzo.
Bado unaweza kujiuliza pia, wachezaji nao wangeweza kuwa na nidhamu kama wanayoonyesha hao wa Afrika Kusini? Wangefanya kazi yao bila ya kuangalia suala la urembo wa huyo dada?
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 ndiyo
imekuwa kipenzi cha Wasauzi na wakati mwingine wanataka ile ya wkaubwa ivunjwe
na hii ya vijana ipewe jukumu la wakubwa.
Chini ya Kocha Owen Da Gama na msaidizi wake, Shaun
Bartlett imekuwa ikiendelea kung’ara.
Jiulize hili kuhusu nchi yetu. Kweli tunakwenda sawa? Kulalamika
ndiyo imekuwa dira katika kila jambo, inatusaidia?
0 COMMENTS:
Post a Comment