Kocha
Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameamua kubwaga manyanga na kuachana na kazi
yake hiyo.
Matola,
nahodha wa zamani wa Simba, alifanya kikao cha saa zima na Rais wa Simba, Evans
Aveva lakini akashikilia msimamo wake.
Taarifa
za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza mambo haya matatu yalichangia Matola
kuachana na Simba.
Moja:
Hawakuwa
wakielewana na Kocha Dylan Kerr katika masuala mengi, jhambo ambalo Matola
aliona kwake lisingekuwa jambo zuri na mwisho angeangushiwa mzigo.
Pili:
Matola
alidai Kerr hakuwa akipokea ushauri wake wa aina yoyote, lakini akafikia hatua
ya kupanga kikosi bila ya kumshirikisha. Wakati mwingine Matola aliijua timu
mbele ya wachezaji wakati wakitangaziwa.
Tatu:
Matola
alianza kuchukizwa kuona Kerr akifanya kikao na wachezaji huku akimtoa yeye
pamoja na staff wengine wa benchi la ufundi, jambo pia aliona si sahihi.
Nne:
Kocha
huyo mzalendo, anamshutumu Kerr kumchonganisha na wachezaji akitaka yeye
kuonekana ni mbaya.
Tano:
Matola
anaamini urafiki wake wa kikazi na Kerr ulianza kuzorota baada ya yeye kushikilia
msimamo wa kutaka kocha Mserbia wa viungo abaki kwa kuwa Simba inamhitaji
lakini taarifa zinaeleza tayari uhusiano wa Mserbia yule na Kerr ulishavurugika
kabisa ndiyo maana wakati anaondoka alisema lazima Simba itafungwa na Yanga,
kweli ikafungwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment