Unaweza ukasema mizozo iko Bongo tu, lakini
sikia hii imetokea England baada ya mmiliki wa timu ya Leyton Orient ya daraja la pili kuamua
kuwapa wachezaji adhabu kwa kuwaweka kambini, tena katika hoteli ya bei rahisi.
Francesco Becchetti ambaye ni mfanyabiashara wa
Kiitaliano, amemuambia Kocha Ian Hendon, timu ikiwa ni pamoja na yeye kocha
waingie kambini kwa kuwa wanafungwa hovyo.
Pamoja na hivyo, mara baada ya kipigo cha mabao
3-1 kutoka kwa Hartlepool, bosi huyo aliamuru timu hiyo isafiri kwa maili 250.
Hoteli hiyo ya Marriott Hotel iliyo katika eneo
la Waltham Abbey, chumba kwa siku ni pauni 100 (zaidi ya Sh 260,000) wakati kila
walipokuwa wakikaa siku moja ya kambi, walikuwa wakilala katika hoteli
inayolipiwa chumba pauni 180 hadi 220.
Uamuzi huo wa Becchetti unatokana na kukerwa na
wachezaji wake kuendelea kuvurunda katika ligi huku yeye akiendelea kugharimika
Hata hivyo, wachezaji wamekuwa wakipewa nafasi
ya kwenda kusalimia familia zao na baadaye kurudi kambini, jambo ambalo kwa
wachezaji na utamaduni wa England ulivyo, wanaona ni adhabu kubwa na kali.
BECCHETTI; BOSI KUBWA LENYEWE |
0 COMMENTS:
Post a Comment