Kocha Charles
Boniface Mkwasa, leo atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
kuzungumzia mechi dhidi ya Algeria ambayo Taifa Stars ilipoteza kwa kutandikwa
mabao 7-0.
Mechi hiyo ya
pili ya kuwania kucheza hatua ya makundi kupambana kwenda Kombe la Dunia 2018
nchini Russia imewaumiza Watanzania wengi kutokana na kipigo hicho.
Jana, Rais wa
TFF, Jamal Malinzi alisema Mkwasa akiwa na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ watazungumza
na waandishi wa habari kuelezea hali hali na mambo yalivyokuwa.
“Kwa kweli kama
TFF tulitoa kila kilichotakiwa, lakini hilo tunamwachia kocha ambaye
atazungumza na waandishi kesho (leo) akiwa na nahodha Cannavaro,” alisema
Malinzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment