November 28, 2015

FARID
Azam FC inalazimika kubadili mfumo wake, kwani winga wake Farid Mussa amepata timu Denmark, hivyo anaondoka  kwenda kufanya majaribio lakini kuna taarifa za kwamba atasajiliwa moja kwa moja.
Kocha wa Azam, Stewart Hall, amesema: “Niwe muwazi kuhusu kinachoendelea kikosini, asilimia 95 nitampoteza Farid Mussa kwani amepata timu Denmark.

“Anatakiwa akafanye majaribio lakini kutokana na uwezo wake, naamini atasajiliwa moja kwa moja, hivyo hapa nina kazi ya kubadili mfumo wa timu ili mambo yaende sawa.”

Kwa kawaida, Mussa hucheza winga ya kushoto katika kikosi cha Azam na Taifa Stars, hivyo Hall kuelekea mechi dhidi ya Simba Desemba 12, mwaka huu anatakiwa kubadili kitu fulani katika mfumo ili mambo yaende.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic