Uongozi wa Azam FC umewajia juu mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara,
Yanga, juu ya taarifa kuwa wanawawania wachezaji wake kadhaa ambapo imewataka
wafuate taratibu za kuwasajili kama kweli wana nia hiyo.
Kumekuwa na taarifa kuwa, Yanga ina mpango wa kuwasajili straika na
beki wa Azam FC, Kipre Tchetche na Pascal Serge Wawa, wote raia wa Ivory Coast
huku ikimuomba kwa mkopo kiungo, Mudathir Yahya.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema kuwa
hawataki kusikia klabu yoyote ikifanya mazungumzo na wachezaji wao katika
kipindi hiki cha mapumziko.
“Kwa sasa wachezaji wetu wote wapo mapumzikoni, naziomba klabu ziache
kuwasumbua wachezaji wetu katika kipindi hiki wakiwa wamepumzika.
“Wao kama wamevutiwa na baadhi ya wachezaji wetu wanatakiwa kuleta
barua ofisini kwetu na siyo kuwafuata kinyemela na kutaka kufanya mazungumzo
bila ya ruhusa ya uongozi.
“Isitoshe uongozi wa Azam hivi sasa upo tayari kumuachia mchezaji
yeyote katika kujenga kikosi imara kitakachochukua ubingwa wa ligi kuu msimu
huu,” alisema Kawemba.
Vipi umeomba ajira Azam nini!?
ReplyDelete