KERR |
Baada ya mshambuliaji wa Mtanzania wa TP Mazembe,
Mbwana Samatta kuibuka mfungaji bora wa Mabingwa Afrika na timu yake
kutwaa ubingwa, kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr amefunguka kuwa straika huyo
anatakiwa kucheza kwa kujiamini kuhakikisha anaibeba Stars dhidi ya Algeria
Jumamosi.
Kerr alisema kuwa Samatta ni moja kati ya
wachezaji wenye vipaji na uwezo wa kufanya vizuri zaidi na amefanikiwa
kumshuhudia akiitumikia timu ya taifa hapa nchini hivyo akishirikiana vyema na
wenzake anaweza kuifikisha mbali Stars.
SAMATTA |
Akiwa Afrika Kusini Kerr amesema mshambuliaji huyo anatakiwa kujituma kwa bidii akishirikiana
na wenzake ili kuweza kuandika historia nzuri zaidi kwa Waarabu hao.
“Samatta nimeona uwezo wake kupitia mechi
za timu ya taifa ya hapa Tanzania lakini ni moja ya vipaji ambavyo nchi hii
inatakiwa kujivunia pia kutokana na kufanya vyema akiwa na klabu yake ya TP
Mazembe sasa ni wakati wa kuonyesha kweli anaweza kwa kuiongoza Stars dhidi ya
Algeria akishirikiana na wenzake.
“Cha msingi anatakiwa kujiamini na ajitume uwanjani
atafanikiwa na kuweza kufika mbali zaidi ya hapo alipo sasa hasa kipindi hiki
ambacho anajukumu zito kuisaidia timu yake ya taifa,”alisema Kerr.
0 COMMENTS:
Post a Comment