HALL (KULIA) AKIWA NA KOCHA WA YANGA, HANS VAN DER PLUIJM. |
Kocha mkuu wa timu ya Azam, Muingereza Stewart Hall
ametoa onyo kali kwa timu zote za ligi ambazo zitakutana na kikosi chake
zijipanga kikamilifu kuweza kuwazuia kwani amepanga kutoa dozi kwa kila timu.
Azam chini ya Stewart imefanikiwa kuwa kileleni mwa ligi
ikiwa na pointi 25 ikifuatiwa na Yanga yenye 23, ambapo katika mchezo ujao wa
ligi kuu Desemba 12, mwaka huu kikosi hicho kitashuka dimbani kumenyana na
Simba katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.
Stewart amesema kuwa kwa sasa hawataangalia aina ya timu
wanayokumbana nayo uwanjani kwani lengo lao ni kuhakikisha wanachukua pointi
tatu za wapinzani wao hao kwa ajili ya kuzidi kujikita katika kilele cha
msimamo wa ligi.
“Kwa sasa hatutaangalia aina ya timu ambayo tunakutana
nayo katika michezo yetu ijayo kwani sisi lengo letu ni moja tu kuhakikisha
tunashinda ili kuweza kuendelea kujiwekea pengo kati yetu na Yanga ambao wapo
nyuma yetu kwa ukaribu.
“Nina uhakika wa kufanya hivyo wa kushinda kila mchezo
wetu kwani kikosi chetu kinaundwa na wachezaji wenye viwango lakini pia wenye
kutaka kushinda katika mechi zetu hivyo haitakuwa shida sana kupata pointi tatu
kwenye mechi zetu,”alisema Stewart.
0 COMMENTS:
Post a Comment