November 10, 2015


Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itakayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.


Michuano hiyo maarufu kama Cecafa Challenge 2015 itafanyika nchini Ethiopia na itaanza kutimua vumbi kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 6 mwaka huu.

Kwa sasa Kibadeni ni mshauri mkuu wa kiufundi katika kikosi cha Taifa Stars kilichoweka kambi jijini Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria, Novemba 14.

Tayari makundi yametangazwa na Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A pamoja na wenyeji Ethiopia, Zambia na Somalia ambalo ni kundi humu.


Kundi B lina timu za Uganda, Burundi na Djibouti wakati Zanzibar iko Kundi C lenye timu za Sudan Kusini, Sudan na Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic