Baada ya kupita siku kadhaa tangu Kocha Msaidizi wa Simba,
Selemani Matola, atangaze kuacha kukinoa kikosi hicho, kocha mkuu wa timu hiyo,
Muingereza, Dylan Kerr, ameibuka na kusema na yeye anaondoka klabuni hapo huku
akidai mechi yake ya mwisho inaweza kuwa dhidi ya Azam FC, Desemba 12.
Matola aliamua kuachana na Simba kwa kile alichoeleza kuwa ni
kutoelewana na Kerr, kwani kocha huyo amekuwa mtu asiyependa kushauriwa.
Ikumbukwe kuwa, wakati Matola anatangaza hivyo, Kerr alikuwa
nchini Afrika Kusini kwa mapumziko baada ya Ligi Kuu Bara kusimama kwa muda
kupisha maandalizi ya timu ya taifa, Taifa Stars, iliyokuwa ikijiandaa na
michezo ya kufuzu Kombe la Dunia.
Kerr alisema Matola hakupaswa
kufanya hivyo, kwani hajui kama uhusiano wake na yeye haupo sawa huku akisema
tangu tukio hilo litokee, vyombo vya habari vimekuwa vikimtupia lawama.
“Vyombo vya habari vimekuwa havinitendei haki, vimekuwa
vikiniandama sana tangu Matola atangaze kuachia ngazi, sasa nimechoka na mimi
nitaondoka.
“Kama nikifungwa na Azam mechi ijayo ya ligi, basi sina haja ya
kubaki na hapo ndipo utakuwa mwisho wangu ndani ya Simba,” alisema Kerr.
Kerr ambaye jana Jumapili alirejea nchini akitokea Afrika Kusini,
wiki hii anatarajia kukiongoza kikosi cha Simba kwenye mazoezi ya kujiandaa na
mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam ambao utapigwa Desemba 12.
0 COMMENTS:
Post a Comment