Michuano
ya Kombe la Shirikisho (AzamHD Federation Cup) inatarajiwa kuendelea leo katika
viwanja vinne tofauti nchini, ambapo kila timu inahitaji kupata ushindi ili
kusonga mbele katika mzunguko wa pili utakaochezwa mwezi Disemba mwaka huu.
Jijini
Mbeya wenyeji Mbeya Warriors watakuwa wenyeji wa Wenda FC mchezo utakaochezwa
uwanja wa Sokoine jijini humo, huku katika uwanja wa Majimaji mjini Songera
timu ya Mighty Elephant watakua wenyeji wa African Wanderes.
Kariakoo ya Lindi
watawakaribisha Changanyikeni FC katika uwanja wa Ilulu, huku timu ya Sabasaba
ya mjini Morogoro wakiwakaribisha jirani zao Mkamba Rangers katika uwanja wa
Jamhuri.
Michuano hiyo itaendelea kesho
Jumatano kwa michezo miwili, Polisi Morogoro watawakaribisha Green Warriors
uwanja wa Jamhuri mjini humo, huku timu ya Mshikamano FC wakiwa wenyeji wa
Cosmopolitan katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Katika michezo iliyochezwa jana,
Abajalo ilibuka na ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Transit Camp, huku Pamba FC
ya jijini Mwanza ikiibuka na ushindi wa bao 1- 10 dhidi ya Bulyankulu FC ya
mkoani Shinyanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment