Kiungo mwenye kasi wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa, amempongeza Mbwana Samatta kutwaa tuzo
ya ufungaji bora Afrika, kwani yeye alijaribu kuitwaa akashindwa.
Ngassa wakati huo akiichezea Yanga mwaka jana,
alifikisha mabao sita katika michuano hiyo akilingana na El Hedi Belameiri wa
ES Setif, Haythem Jouini (Esperance) na Ndombe Mubele wa AS Vita.
Kwa kuwa hakushiriki mchezo wa fainali, Ngassa
alikosa tuzo hiyo ya mfungaji bora japokuwa jina lake limo kwenye orodha ya wafungaji
bora msimu huo wa 2014.
Ngassa amesema: “Nilijaribu kuwa mfungaji bora
mwaka jana, lakini mambo yakashindikana ila mwenzangu Samatta ameweza, hongera
kwake.”
Wikiendi iliyopita, Samatta akiichezea TP
Mazembe, alifunga bao moja na kufikisha mabao saba huku akitengeneza lingine na
kuiwezesha timu yake kushinda mabao 2-0 dhidi ya USM Alger katika mechi ya
fainali ya marudiano jijini Lubumbashi, DR Congo.
Mazembe ilitwaa ubingwa huo wa Ligi ya Mabingwa
Afrika huku Samatta akipewa tuzo ya ufungaji bora.
0 COMMENTS:
Post a Comment