November 14, 2015

TUMBA (KULIA) AKIMDHIBITI RAMADHANI SINGANO WAKATI AKIWA SIMBA.

Klabu ya Mbeya City inapambana kumsajili beki wa kati wa Coastal Union, Tumba Sued, ili azibe kikamilifu nafasi ya Juma Nyosso aliyefungiwa kucheza soka kwa muda wa miaka miwili.


Nyosso hivi karibuni alifungiwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kosa la kumdhalilisha straika wa Azam FC, John Bocco.

Hata hivyo, Mbeya City itabidi itumie nguvu ya fedha ili kumpata Tumba kwani amebakiza miezi miwili kumaliza mkataba wake na Coastal wakati dirisha la usajili linafunguliwa kesho Jumapili Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union, Salim Bawaziri, amethibitishia kuwa kweli Mbeya City inamtaka beki huyo japokuwa nao bado wanamhitaji.

 “Tumba amekuwa msaada kwenye timu na bado tunamhitaji, tumeongea naye amekiri kuwa Mbeya City wanamuhitaji pamoja na Ndanda FC, tutahakikisha anabaki,” alisema Bawaziri.


Bila kumtaja Tumba, Kocha wa Mbeya City, Meja Mstaafu Abdul Mingange alisema klabu yake inasaka mbadala wa Nyosso ili wafanye vizuri katika mechi zijazo japokuwa wapo Yohana Morris na Christian Sembuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic