November 2, 2015




Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza wachezaji 10 wa mwisho watakaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika 2015.11.02, badala yake limemuacha awanie tuzo kwa wachezaji bora wanaocheza barani Afrika.
Ajabu Caf katika wachezaji hao 10, ni mmoja pekee anayecheza soka barani Afrika huku likimuacha mshambuliaji nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta aliyeiongoza TP Mazembe ya DR Congo kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mchezaji pekee wa Afrika aliyechukuliwa ni Mudather Altaib Ibrahim ‘Karika’ wa Al Hilal ya Sudan ambayo haikufika fainali.
Yaya Toure wa Ivory Coast anayetetea tuzo hiyo akitokea Man City ya England, Adre Ayew wa Swansea, Mohammed Salah wa AS Roma na Yacine Ibrahimi wa FC Porto na Algeria ni kati ya 10 waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo.


LISTI KAMILI YA HAO 10 WALIOCHAGULIWA...


 TIMU
TAIFA
Andre Ayew
Swansea City
Ghana
Aymen Abdennour
Valencia
Tunisia
Mudather Eltaib Ibrahim 'Karika'
Al-Hilal
Sudan
Mohamed Salah
Roma
Egypt
Pierre-Emerick Aubameyang
Borussia Dortmund
Gabon
Sadio Mane
Southampton
Senegal
Serge Aurier
Paris Saint-Germain
Ivory Coast
Sofiane Feghouli
Valencia
Algeria
Yacine Brahimi
Porto
Algeria
Yaya Toure
Manchester City
Ivory Coast

1 COMMENTS:

  1. Samatta yupo katika orodha ya wachezaji kumi bora- based in Africa. Ni category ambayo aliingia tangu awali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic