Yanga imeshindwa kuingia kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara kutokana na michuano ya Kombe la Chalenji iliyopangwa kuanza Novemba 20 jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Yanga hivi sasa inaendelea na maandalizi ya ligi kuu
chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van Der Pluijm na Juma Mwambusi wakati ligi
hiyo ikisimama.
Pluijm amesema ni
ngumu kuifuata programu aliyoipanga wakati ligi kuu ikisimama kutokana na nusu
ya wachezaji kuwepo vikosi vya timu zao za taifa.
Pluijm alisema, katika ripoti yake aliomba mechi tano
za kirafiki za kimataifa pamoja na kambi ya pamoja ya kujiandaa na ligi hiyo
katika kuhakikisha wanautetea ubingwa wao.
“Timu inaendelea na mazoezi yake ya pamoja ikiwa na
mchanganyiko wa wachezaji wa U20 baada ya nusu ya wachezaji wa timu kubwa
kuwepo kwenye timu zao za taifa.
“Hivyo hivi sasa siwezi nikafanya chochote ikiwemo
kucheza mechi za kirafiki za kimataifa, pamoja na kambi ya kujiandaa na ligi
kuu iliyosimama hadi pale wachezaji wote watakaporejea kujiunga na wenzao,”
alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment