Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ameweka wazi
kuwa, ratiba ya ligi imekuwa ni kikwazo kwake cha kuandaa program za muda
mrefu.
Kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi yake ikiwa na wachezaji
wachache wa kikosi cha kwanza kutokana na wengi wao kuwepo katika timu zao za
taifa kwa ajili ya michuano ya Chalenji inayofanyika mjini Addis Ababa,
Ethiopia.
Pluijm alisema kuwa anaweza kusema kuwa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) limekuwa likipanga ratiba ya ligi vibaya ambapo huwa inavuruga
utaratibu mzima wa uboreshaji wa timu.
“Nashangaa TFF sijui wanapangaje ratiba yao, ligi inasimamasimama
bila mpangilio, wachezaji wanatumika sana nje ya klabu zao, hii ipo tofauti
kabisa na nchi nyingine ulimwenguni.
“Ratiba hii inaharibu kabisa programu zangu kwani kwa kipindi
kirefu huwa nawakosa wachezaji wangu muhimu, hivyo siwezi kuwapa mbinu za
kupambana katika ligi ili tuweze kuwa mabingwa mwishoni mwa msimu.
“Kama kipindi hiki ligi imekolea lakini tumelazimika kusimama ili
wachezaji wetu waende kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu
Kombe la Dunia, mechi zimeisha wanaenda Ethiopia kwa ajili ya Michuano ya
Chalenji, hapa sitaweza kabisa kukipa mazoezi kamili kikosi changu chote kwa
kuwa wengi wao wa kikosi cha kwanza hawapo,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment