November 1, 2015


Mtanzania Mbwana Samatta ameiweka klabu yake ya TP Mazembe katika nafasi nyingine ya kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufunga bao muhimu.
TP Mazembe imeshinda kwa mabao 2-1 katika mechi yake ya kwanza ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya USM Alger 2-1.
Licha ya kuwa ugenini, TP Mazembe ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Rainford Kalaba katika dakika ya 27 lakini dakika ya 45 Mzambia huyo akatolewa kwa kadi nyekundu.
Kipindi cha pili, TP Mazembe walionyesha kuwa makini wakilinda lbao lakini walimtumia Samatta kuendelea kuwasumbua walinzi wa USM Alger.
Dakika ya 68, Hocine El Orfi alilambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu.
Dakika ya 79, Samatta akafanya yake baada ya kufunga bao la pili na kuiweka Mazembe katika nafasi nzuri kabla ya mechi ya marudiano Novemba 8 mjini Lubumbashi.

Hata hivyo wenyeji walionekana kutokata tamaa hadi walipopata bao moja katika dakika ya 88 kupitia kwa Mohammed Seguer.

1 COMMENTS:

  1. MKWASA ANAPASWA KUWATUMIA MSUVA NA TELELA
    Nimeangalia michezo yote ya STARS tangu mkwasa alipokabidhia timu ya taifa. Yapo mambo baadhi ambayo niliyagundua na nimeona nami kama mtanzania nitoe mchango wangu angalau wa maneno. Timu yetu inatatizo kubwa sana la kiungo na japo si sana Beki wa kati. Viungo tulio nao wengi wao wanakosa nguvu na uzoefu. mfano. Mkwasa amekuwa akiwatumia ndemla na mdathiri yahya. Vijana hawa ni wachezaji wazuri lakini wanakosa nguvu na uzoefu kutokana na maumbo yao kuwa madogo. Himid Mao kwa mtazamo wangu ni chaguo sahihi. Huyu dogo ana vitu vinavyotakiwa kwa mchezaji. Ana nguvu, akili na ni mkorofi pale ambapo adui anatishia usalama wa goli lake japo anatakiwa ashauriwe kuongeza bidii. Katika mchezo zidi ya nigeria, Ndemla na Mdathiri walicheza vizuri lakini kwa mtazamo wangu, mchcezo huu sio kipimo sahihi kwa STARS kwani wachezaji wengi wa nigeria tunaowajua si wale waliokuja, wangeweza kufungwa na timu yoyote ile. ikumbukwe kwamba, hao hao nigeria walifungwa na Uganda hivi majuzi tu goli moja bila. Katika mechi yetu na Malawi, Kiungo chetu kilipwaya kabisa katika michezo yote miwili. japo mchezo wa kwanza tulishinda, hiyo ilikuwa bahati ya mwenyezi mungu maana malawi walicheza vizuri zaidi yetu. Nilimsikia mkwasa akisema jamaa walikuwa hawatupi nafasi lakin Nigeria wanacheza open footbal; Hii siyo kweli kabisa. usitegemee Algeria kukupa nafasi wakati wanatafuta ushindi. Kama tukiendelea kuamini kwamba eti kiungo chetu ni bora na kwamba kilipwaya kwa sababu Malawi walitunyima nafasi ya kucheza, tusitegemee lolote kutoka kwenye mechi na algeria. Nimemuona TELELA kwenye mechi za yanga. ana nguvu, ana akili na anaweza kupiga. ni vizuri mkwasa akawachezesha katikati na MAO.
    MSUVA. Pamoja na madhaifu aliyonayo msuva, ana faida zifuatazo; anaweza kukaba, ana nguvu, ana mbio na pasi zake zina macho hasa cross. pia anaweza kupiga na anapokaribia gori huwa anatulia.
    Ngasa. Ni mchezaji mzuri lakini ana papara sana. si shauri ngasa kuanza wakati msuva yuko benchi. siamini kama zile nafasi alizozikosa ngasa katika mchezo wa nigeria, msuva angeweza kuzikosa. kiufupi ngasa alitunyima ushindi.
    FARIDI MUSA: Dogo huyu ni hadhina sana kwa soka letu endapo ataendelea hivyo. Dogo huyu ana Mbio, ana nguvu anaweza kupunguza mabeki wawili-watatu na anajua kupiga pasi za kuchopu. Hebu angalia michezo yote aliyocheza kwenye timu yake na kwenye timu ya taifa harafu hesabu pasi zake zilizopotea utakuta ni chace mno. Kwa mtazamo wangu, nadhani tunashindwa kumfaidi vilivyo kwa sababu ya kumchezesha pembeni. Ningekuwa mimi Kocha, nimgemweka namba kumi karibu na SAMATTA harafu msuva na ulimwengu wakicheza kulia na kushoto . uwezo wake wa kupunguza mabeki wawili watatu na kupiga pasi za kuchopu kungemuweka vizuri samata kutupia mabao mengi. anaweza kujaribiwa angalau kwa dk.15 asipoleta matunda basi anabadilishwa. Hata hivyo anappaswa kushauriwa ajiamini zaidi akijifunza kwa kaka yake samatta. sio kila mpira ni wa kupiga kross. wakati mwingine unatakiwa kuchukua maamuzi magumu ya kupunguza mabeki na kuingia ndani ya kumi na nane harafu ndipo ufanye maamuzi yenye matunda kwa timu. Huo ndo mchango wangu lakini kocha aweza kuamua mwenyewe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic