Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa, amefunguka
juu ya yaliyotokea nchini Algeria walipoenda kucheza mchezo wa marudiano wa
kusaka nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa hilo.
Stars ilipata kichapo cha mabao 7-0 katika mchezo huo wa
pili, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 9-2. Akizungumza na Championi Ijumaa,
Mkwasa alielezea yaliyowatokea kiasi cha kuonekana ni kama walipoteza mchezo
hata kabla ya kuingia uwanjani.
Mkwasa anatiririka: “Kwanza tulipotua Algeria, walianza
kufanya fitina palepale uwanja wa ndege, tulikuta wenyeji wametuandalia basi
ambalo tulilikataa kwa kuwa kuna basi lingine tuliandaliwa na mtu tuliyemtuma.
“Ubishani wa suala hilo ulichukua muda mrefu, mwisho
tukapanda lile ambalo tuliandaliwa na mtu wetu, tukachelewa kufika hotelini,
siku hiyo ikaisha bila ya kufanya mazoezi.
“Katika mkutano wa kabla ya mechi (pre match meeting),
walikuwa wakitumia Lugha ya Kiarabu na Kifaransa, tukaomba mtu wa kututafsiria
wakagoma.
“Tulipoingia uwanjani wakati wa kupasha kabla ya mechi,
upande wetu pekee ndiyo ukawa umemwagiwa maji huku ule mwingine ukiachwa, ndiyo
maana wakati wa mchezo tukawa tunateleza, kwa kuwa wenzetu walikuwa na viatu
maalum vyenye meno makali, wakawa hawatelezi.
“Wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania unaimbwa, mashabiki
wa Algeria walikuwa wakizomea kitendo ambacho si cha kiungwana.
“Tukiwa mapumziko, upande wetu ukawa unamwagiwa maji
kama awali ilivyokuwa. Tuliporudi uwanjani tulikuta upande wetu umemwagiwa maji
kama ilivyokuwa awali, kwa kweli wachezaji wangu walipata shida sana na
ukichanganya na kukataliwa kwa bao la Maguri (Elias), kila mmoja alikata tamaa.
“Wao wanapokuja huku sisi tunakuwa wakarimu kupitiliza
wakati tukienda kwao wanatufanyia fitina mwanzo mwisho.”
Sidhani kama kweli ni sababu za ukweli ambazo amezitoa master namjua ni mtu makini na mkweli nadhani ataeleza sabubu za kiufundi zaidi siyo hizo polojo za waandishi.
ReplyDelete