Na Saleh Ally
Simba ni kati ya timu zilizoanza mazoezi kujiandaa
zaidi na Ligi Kuu Bara ambayo ilikuwa imesimama.
Kwa sasa imefikisha kama wiki moja ikifanya mazoezi
chini ya Dylan Kerr anayesaidiana na Kocha Mkenya, Iddi Salim.
Pamoja na maandalizi ya mapema, Simba inaonekana ina
kikosi cha vijana wengi ambao si wanaotumika katika Ligi Kuu Bara.
Mazoezi hayo ni mazuri lakini kimahesabu inaonekana
walengwa hasa, hawako pamoja na timu.
Ingawa wachezaji wawili au watatu wako katika kikosi
cha Taifa Stars na wengine wamechaguliwa Kili Stars, bado inaonyesha mazoezi ya
Simba, hayatakuwa na faida kubwa kwa kikosi cha kwanza.
Huenda Kerr ameamua kuanza mapema akitaka kujipanga na
kurekebisha kikosi. Lakini ukweli bado inaonekana malengo yake hayawezi
kutimia.
Kama Simba itaendelea na mazoezi na kikosi hicho kwa
wiki moja au zaidi. Hakika malengo ya kocha huyo na msaidizi wake, kamwe
hayawezi kufikiwa.
Ukiangalia picha hiyo ina wachezaji wapatao 10, kati
ya hao, makipa wawili ndiyo wenye nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza pamoja na
viungo washambuliaji wawili, Mussa Hassan Mgosi na Joseph Kimwaga ambao katika
uhalisia si wenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.
Hesabu inaonyesha kati ya 10 unaowaona katika picha
angalau wachezaji wawili tu wanaweza kuwa na uhakika wa namba katika kikosi cha
kwanza. Utapima mwenyewe.
Jambo zuri ni kwa wachezaji wengi wa Simba kuhakikisha wanawahi mazoezi mara moja kila wanapotakiwa kufanya hivyo.
Kuwahi ni kumsaidia kocha kutekeleza anachotaka kufundisha kwa upanda badala kuendekeza 'ubishoo' wa kuonekana mjanja au staa ni yule anayechelewa kuripoti.
Pia wachezaji wanapaswa kuonyesha ukubwa wa nidhamu yao, kuachana na kufanya mambo kwa mazoezi, zamani ilionekana ni kitu cha kawaida. Lakini sasa vitu vimebadilika.
0 COMMENTS:
Post a Comment