Kocha mwenye mbwembwe nyingi, Zdravko Logarusic kwa sasa
yupo nyumbani kwao Croatia baada ya kuzinguana na Wakenya wa FC Leopards,
sasa anasema anasaka timu popote pale hata iwe timu yake ya Simba iliyomtimua
ya Simba.
Ikumbukwe kuwa Loga alitimuliwa na Simba mwishoni mwa
msimu wa 2013/14, katika maandalizi ya msimu uliopita na timu kupewa
Mzambia, Patrick Phiri ambaye pia alitimuliwa ndani ya mechi nane, kisha kuwa
mikononi mwa Mserbia, Goran Kopunovic kabla ya kukabidhi kijiti kwa Muingreza,
Dylan Kerr.
Akizungumza kutoka Croatia, Logarusic
alisema licha ya Simba kumtimua anaamini ni sehemu ya maisha ya ukocha na
kwamba yupo tayari kurejea kikosini hapo.
Ameongeza kuwa mbali na hilo, pia bado anaipenda maisha
ya Tanzania kutokana na kujaliwa vipaji vya soka.
“Kwa sasa niko Croatia ninapumzika, sina timu, lakini
nikipata ofa popote pale nipo tayari kufanya kazi. Hata kama ni kurudi Simba
nipo tayari maana sina uhasama nao, sema ni sehemu ya maisha ya ukocha
kuachishwa kazi. Naipenda Tanzania, nafurahia sana maisha ya hapo kutokana na
kujaliwa kuwa na vipaji vya soka. Kweli naipenda Tanzania,” alisema Logarusic.
0 COMMENTS:
Post a Comment