| WAWA |
Siku
chache baada ya kiungo mshambuliaji Brian Majwega, raia wa Uganda, kutua Simba,
amefunguka kuwa amepania kuonyesha uwezo wa juu huku akijinadi kuwa ameshamwaga
siri za kumzima beki kisiki wa Azam FC, Paschal Wawa.
Majwega
amejiunga na Simba hivi karibuni ambapo awali alikuwa akiitumikia Azam, usajili
wake umekuwa gumzo hasa kwa kuwa Azam bado imesema kuwa ina mkataba naye.
Wakati
hayo yakiendelea, Majwega ameliambia Championi Ijumaa kuwa, amepanga kuonyesha
kiwango kikubwa kama akipewa nafasi katika mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara ambayo
itazikutanisha timu hizo mbili mnamo Desemba 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
“Naamini
TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) itanipa haki yangu kwa kuwa mimi ndiyo nipo
sahihi tofauti na Azam, pia siyo kwamba nitaihofia Azam tutakapokutana,
nikipewa nafasi nitafanya makubwa na kuhakikisha naisaidia Simba kushinda siku
hiyo.
“Kuhusu
Wawa najua cha kufanya kwa beki kama huyo ambaye anawadhibiti halafu anapanda
kuja kushambulia. Kwanza ni kuwazonga langoni mwao muda wote ili asipate nafasi
ya kujipanga lakini vitu vingine nitaongea na wachezaji wenzangu na tutajua
nini cha kufanya,” alisema Majwega.
SOURCE:
CHAMPIONI







0 COMMENTS:
Post a Comment