November 27, 2015

   
DE WIJS.

Mjukuu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ameendelea kula shavu katika Klabu ya PSV Eindhoven inayoshiriki Ligi Kuu ya Uholanzi.


Mjukuu wake huyo anayejulikana kwa jina la Jordy De Wijs, mwenye umri wa miaka 19, ameongeza mkataba na klabu hiyo juzi kwa mkataba wa miaka minne hivyo ataitumikia mpaka 2019. PSV iliifunga Manchester United, mwezi uliopita na juzi timu hizo zilitoka suluhu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester United.
PLUIJM

Pluijm alisema amefurahishwa na hatua hiyo ya mjukuu wake na ana imani naye kwamba atafanya vizuri zaidi kwa kuwa ana uwezo wa kucheza pia kama beki wa kati, kiungo mkabaji na kiungo cha ushambulizi pia.
....AKIWA KAZINI.


“Nilikuwa nikimuona alivyokuwa akijitahidi kupambana uwanjani tangu akiwa mdogo, pia hakuwa mtu wa kukata tamaa inawezakana hali hiyo ndiyo imemfanya afike hapo. Anacheza nafasi mbalimbali uwanjani lakini zaidi ni mzuri akicheza kama beki wa kati au wa kushoto,” alisema Pluijm.

Katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSV Eindhoven imekuwa ikiisumbua Man United kinoma.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic