Azam FC imezidi kujichimbia katika nafasi ya pili baada ya kuongeza pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu Bara.
Azam FC imeongeza pointi hizo baada ya kuitwanga Majimaji kwa mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Kikosi hicho cha Azam FC kilipata mabao yake mawili katika kipindi cha kwanza kupitia Ame Ali na Didier Kavumbagu katika dakika za 10 na 20.
Hata hivyo hali ya uwanja ilikuwa hovyo kutokana na mvua zilizonyesha mchana kutwa.
Mara kadhaa, mpira ulikwama kwenye madimbwi kutokana na maji na matope kujaa uwanjani.
Kwa ushindi huo, Azam FC unefikisha pointi 29 nyuma ya Yanga iliyo kileleni ikiwa na pointi 30.







0 COMMENTS:
Post a Comment