Kali hali isiyokuwa ya kawaida, wachezaji wa Simba wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki wa Ndanda wakati wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona mjini Mtwara, jioni hii.
Kabla ya hapo, wachezaji wa Simba walilazimika kusubiri kwa zaidi ya saa moja baada ya uongozi wa Uwanja wa Nangwana kugoma kuwafungulia mlango.
“Baada ya juhudi za ziada, mlango ulifunguliwa kwa kuwa ni sheria kwamba tunaruhusiwa kuutumia siku moja kabla ya mechi.
“Ajabu tulizuiwa, baada ya juhudi binafsi ukafunguliwa na wakati tunaanza mashabiki hao nao waliingia na kuanza kuporomosha matusi makali sana.
“Wachezaji walikuwa wavumilivu wakaendelea na mazoezi, wale watu wakahama pale na kwenda jukwaani. Kule walikaa nako wakaendelea kutukana sana, bado kila mtu alikuwa mvumilivu,” alieleza mmoja wa watu walioongoza na kikosi cha Simba mjini Mtwara.
“Baada ya kumaliza mazoezi wakati tunatoka, ndipo wakaanza kurusha mawe katika basi na magari mengine. Baadhi ya watu wakashuka na kuanza kuwakimbiza.”
“Kwa kweli tumefanyiwa vurugu sana, unyanyasaji wa wazi na hiki ni kitu cha ajabu kabisa.”
Simba inatarajia kushuka dimbani kesho kuivaa Ndanda pia ni haki yao kuutumia uwanja huo kwa mazoezi yao leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment