Na Saleh Ally
Timu tatu za Ulaya zinamtaka mshambuliaji
Mbwana Samatta wa TP Mazembe na zinatokea katika nchi mbili za Ufaransa na Ubelgiji.
Samatta amefanya mahojiano na Championi Jumatatu
na kusema tayari timu hizo zimeweka ofa mezani, hivyo ni kazi kwake kuchagua
aende wapi.
Lakini hata hivyo amefikia uamuzi mmoja,
kwamba sasa hatasaini na klabu yoyote kuichezea timu tatu kati ya hizo hadi
baada ya michuano ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu itakapomalizika.
SALEHJEMBE: Kumekuwa na uhakika wa taarifa
za kuondoka TP Mazembe, lakini hakuna uhakika unakwenda wapi!
Samatta: Kama ni kwa sasa, basi ninaweza
kwenda kati ya nchi hizi, Ufaransa au Ubelgiji.
SALEHJEMBE: Ni kwa ajili ya majaribio?
Samatta: Majaribio niliishakataa ni kwenda
kusaini. Hapa nilipofikia sidhani kama ninahitaji majaribio. Labda kama ni zile
timu kubwa sana, hapo ningeweza kufanya.
SALEHJEMBE: Ni timu ngapi zimejitokeza
kukupa ofa na unatarajia kusaini lini baada ya kuichagua ipi?
Samatta: Ofa tatu ziko mezani, kuchagua ipi
ni suala la baadaye kwa kuwa nimeona nisisaini sasa.
SALEHJEMBE: Unataka kusaini lini na kwa
nini?
Samatta: Tayari ofa ziko mezani, hivyo
kuchagua ni rahisi tu, lakini nimeona nisisaini kwa sasa ili nifanye hivyo
baada ya Kombe la Dunia kwa klabu.
SALEHJEMBE: Kombe la Dunia linazuia vipi
usisaini wakati ofa iko mezani na uongozi wa TP Mazembe umekubali uende?
Samatta: Hauwezi kujua kitakachotokea katika
michuano hiyo, kama ni neema ninaweza kupata klabu nyingine kubwa zaidi. Subira
si jambo baya.
Awali kabla ya ofa hizi ilishatangazwa kuwa
Samatta anaweza kujiunga na Lille ya Ufaransa baadaye mwezi Januari.
0 COMMENTS:
Post a Comment