December 14, 2015

SHIME

Kocha Mkuu wa Mgambo JKT, Bakari Shime, amemponda beki wa Yanga, raia wa Togo, Vincent Bossou kuwa ni mchezaji wa kawaida sana na ambaye anapitika kirahisi mno.

Shime amesema kuwa katika mechi ya juzi Jumamosi, kama wasingekuwa Kelvin Yondani na Mbuyu Twite, basi Yanga ingeambulia kichapo katika mechi hiyo, tena kisichopungua mabao matatu.

Alisema katika mechi hiyo, Yondani na Twite walifanya kazi kubwa sana ya kuzuia mashambulizi ya washambuliaji wake, tofauti na ilivyokuwa kwa Bossou.
BOSSOU AKIWA BENCHI PAMOJA NA KIPA DIDA

“Nawapongeza sana vijana wangu kwa kazi nzuri waliyoifanya uwanjani, walijitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanaibuka na ushindi lakini mambo hayakuwa mazuri kutokana na ukuta wa Yanga kusimama imara.


“Wachezaji Yanga waliotupatia tabu sana na kutufanya tusipate bao hata moja ni Twite na Yondani, walifanya kazi kubwa sana ya kuvuruga mipango yetu lakini yule Mtogo wao alikuwa hatishi na mara nyingi vijana wangu walikuwa wakimpita tu,” alisema Shime.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic