December 14, 2015


Wimbi la majeruhi limezidi kukiandama kikosi cha Yanga ambacho kwa sasa kipo jijini hapa kikijifua kwa ajili ya mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Sports.

Baada ya hivi karibuni kikosi hicho kuwakosa nyota wake watatu ambao ni Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mzimbabwe, Donald Ngoma kutokana na majeraha, pia kitamkosa kiungo wake kiraka, Salum Telela kwa zaidi ya wiki mbili.

Kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Haruni Ally, Telela atakuwa nje ya uwaja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu yaliyokuwa yakimsumbua mara kwa mara na kumfanya ashindwe kucheza soka kama inavyotakiwa.

“Hali ya majeruhi katika kikosi chatu siyo mbaya sana ila ameongezeka mwingine ukiachana na Joshua, Ngoma na Cannavaro, huyu mwingine ni Telela ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo.

“Anasumbuliwa na matatizo ya kifundo cha mguu kwa muda mrefu, hivyo baada ya mimi kujiunga na Yanga nilipewa jukumu la kuwaangalia wachezaji wanaokuwa wakiumia kila wakati ili niweze kuyapatia ufumbuzi matatizo yao.


“Baada ya kumfanyia vipimo vya MRI, ndipo tukagundua kuwa ana tatizo kubwa ambalo litamfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo,” alisema Ally.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic