Na Saleh Ally
Nakukumbusha kwanza, Yanga imezaliwa mwaka 1935 na ndiyo
ilimeguka na kuanzishwa kwa Simba ikianza kwa jina la Stanley.
Yanga ya miaka 25 iliyopita, inaonekana iliweza kwa wakati zaidi
kuliko Yanga ya sasa.
Sasa Yanga ndiyo mabingwa, lakini ndiyo waliobeba mara nyingi
zaidi ubingwa wa Tanzania Bara. Wamechukua mara 25 kati ya 50, wanastahili
pongezi.
Ubingwa waliochukua Yanga ni wa soka, si mchezo mwingine. Lakini
nembo ya Yanga inaonyesha ni klabu ya michezo mbalimbali ikiwemo netiboli.
Soka ni sehemu, nembo inaonyesha kuna bondia na netiboli.
Michezo yote inahusisha wanaume na wanawake kama ilivyokuwa awali.
Tena kama ni michezo mbalimbali, basi wanaume na wanawake lakini
kila upande unatakiwa kuwa na vijana.
Lakini ukweli ni hivi; Yanga sasa imebaki kuwa timu au klabu ya
soka pekee na kilichobaki ni majungu na watu kutopendana.
Watu kutosikilizana, hata kama mambo yanakwenda vizuri, wako
ambao hawasikilizani na wenzao na kila mara wanalalamika.
Hao ndiyo wale wanaotofautiana na ule mwenge wa kwenye nembo ya
Yanga ambao inataka Wanayanga kuwa pamoja na kumulika pamoja.
Lakini Yanga si klabu ya soka pekee, inawezekana hata viongozi
wa klabu hiyo hawajui. Vipi wazee wa enzi hizo, waliweza kushirikisha michezo
kibao hadi timu ya mchezo wa ngumi na waliopo sasa washindwe?
Kipindi hicho hadi timu za watoto, vijana, kinadada na leo
hakuna zaidi ya ile ya soka! Tatizo ni nini?
Jiulize, kwani viongozi wa Yanga hawajahi kuiangalia logo hiyo
ambayo ika karibu kila sehemu ikiwa ni pamoja na pale katika makao makuu ya
Yanga mitaa ya Jangwani na Twiga?
Nembo inaonyesha ni timu ya michezo mingi, klabu ya watu na
washiriki wa michezo mingi lakini waliopo sasa kwa kuwa wanapenda soka pekee,
wameigeuza Yanga kuwa klabu ya soka na kufuta kwa makusudi rekodi ya historia
zake kwamba ni klabu ya michezo inayojumuisha wanamichezo na si wapenda soka
pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment