Kumbe Selemani Matola anajua, leo timu yake ya daraja la pili ya Bulyanhulu Gold Mine imeitoa shoo Simba ya Dylan Kerr.
Kikosi cha Matola kimeshinda kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa mjini Geita.
Mabao hayo matatu ya Bulyahulu yalifungwa na Kaisi Pastory, Juvenary Pastori na Emmanuel Swita.
Matola aliondoka Simba baada ya kutangaza kushindwa kufanya kazi aliyekuwa bosi wake, Kerr.
Soka lilikuwa la kuvutia na Simba ilianza kutawala mchezo kabla ya kikosi cha Matola kuanza kuchukua usukani taratibu.
Simba ambao wako njiani kwenda Shinyanga kuwavaa Mwadui FC walishindwa kutumia nafasi kadhaa ambazo zingeweza kuwapatia angalau mabao mawili.







0 COMMENTS:
Post a Comment