December 21, 2015


Ushindi raha bwana, baada ya Yanga kufanikiwa kuifunga Stand United kwa mabao 4-0 juzi Jumamosi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amediriki kusema hiyo ni mechi bora ya msimu mpaka sasa.

Yanga ilitoa kipigo hicho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kuzidi kujikita kileleni kwa jumla ya pointi 30 baada ya michezo 12, ikifuatiwa na Azam yenye 26 kabla ya mchezo wao wa jana, kisha Mtibwa wenye 24.

Akizungumzia mchezo huo, Pluijm alisema si kwamba amefurahishwa na ushindi mnono wa mabao hayo pekee, lakini pia alikunwa na soka safi lililopigwa na vijana wake hao waliofanikiwa kuonyesha kiwango cha juu siku hiyo.

Aidha, pia aligusia kufurahishwa na mshambuliaji wake, Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye hakufunga lakini alitoa asisti za mabao mawili yaliyofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe.

“Ilikuwa mechi nzuri, naweza kusema ni mchezo wetu bora zaidi wa msimu mpaka sasa, sijui mechi zinazofuata lakini kwengu ni mechi bora zaidi, achana na ushindi wa mabao manne lakini kiwango chao ndani ya uwanja pia kilikuwa juu, walicheza kwa pasi safi na kuonana vizuri.

“Ngoma hakufunga lakini alifanya vitu vingi vizuri zaidi, alimwangalia Tambwe kila wakati na tukapata mabao mengi, nimefurahishwa na hilo, naamini tutaanzia hapo katika kupanda juu zaidi,” alisema Pluijm.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic