December 21, 2015


Mshambuliaji Simba, Danny Lyanga amesema anajivunia kuwemo katika kikosi cha Simba ambacho kitakuwa na mabadiliko makubwa.

Lakini amewataka mashabiki wa Simba kutokatishwa tamaa na matokeo ya mechi dhidi ya Toto African ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, juzi.

Katika mechi hiyo Simba iliruhusu bao la 'usiku' kabisa kutokana na uzembe wa beki wake Hassan Isihaka kushindwa kuruka na kupiga kichwa mpira uliomfikia straika wa Toto aliyefunga kwa ulaini kabisa.


“Najivunia kuwepo Simba ambako kuna wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa lakini matokeo dhidi ya Toto yalitokana na uwanja kujaa maji na matope.”

Lyanga amekuwa nguzo ya ushambulizi ya Simba katika mechi mbili tu alizocheza ambazo amefunga bao moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic