Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe ametamba kuwa ana uwezo wa kuendelea kufanya vizuri.
Tambwe amesema anaamini anaweza kufunga hat trick zaidi na kuchukua mipira lakini ikishindikana, hatalazimisha.
“Kiuchezaji hauwezi kujua lini utafunga hat trick, lakini kila inapowezekana, basi unafanya.
“Kama imeshindika haulazimishi kwa kuwa kikubwa ni ushindi kwa timu ambayo ni mafanikio ya wote. Kama haufundi unatengeneza kwa wenzako,” alisema Tambwe.
Tambwe amefunga hat trick kwa misimu yote mitatu ambayo amechea soka nchini.
Katika mechi ya Stand United alifunga mabao matatu na Yanga ikashinda kwa mabao 4-0







0 COMMENTS:
Post a Comment