Uongozi wa Yanga, umetangaza kuvunja mkataba wake na kiungo wake Haruna Niyonzima.
Yanga imechukua uamuzi huo ikiwa ni miezi isiyozidi mitano tokea isaidi mkataba mpya wa miaka miwili na Niyonzima.
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema Niyonzima atalazimika kulipa kiasi cha dola 71,175 (zaidi ya Sh milioni 149) kutokana na kukiuka mkataba uliosababisha kuvunjika kwa mkataba huo.
Mzozo wa Yanga na Niyonzima ulianza baada ya kiungo huyo kuchelewa kurejea kazini alipokwenda kuitumikia timu yake katika michuano ya Chalenji nchini Ethiopia.
Uongozi wa Yanga ulimsimamisha kwa madai amekuwa na tabia hiyo ya kuchelewa kila mara na kumtaka atoe maelezo.
“Lakini hata hayo maelezo hakuwasilisha kama ambavyo alitakiwa kufanya. Mwisho hiki ndicho uongozi wa Yanga umeamua kuchukua,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment