January 25, 2016


Kikosi cha Azam FC, leo Jumatatu usiku kinatarajia kusafiri kuelekea nchini Zambia kwenda kushiriki mashindano maalumu yaliyoandaliwa na mabingwa wa nchi hiyo, timu ya Zesco ambapo pia TP Mazembe ya DR Congo itashiriki.

 Msemaji wa timu hiyo, Jaffar Idd Maganga, alisema wanakwenda nchini humo baada ya kupokea mwaliko maalumu kutoka kwa timu ya Zesco.

“Kesho (leo Jumatatu) kikosi chetu chote kinatarajia kusafiri kuelekea Zambia kwenda kushiriki mashindano maalumu tuliyopewa mwaliko na mabingwa nchi hiyo, timu ya Zesco ambayo anaitumikia Mtanzania, Juma Luizio.

“Mwaliko huo siyo wa kwanza kwetu kwani kama unakumbuka tuliwahi kwenda Congo kipindi cha nyuma tulipoalikwa na TP Mazembe ambao pia tutacheza nao.

“Tumeuchukulia siriazi mwaliko huo kwani kama unavyofahamu huko tunaenda kukutana na mabingwa kutoka nchi mbalimbali, hivyo na sisi tunaenda tukiwa tumejipanga vilivyo na tutayatumia mashindano hayo kama sehemu ya maandalizi yetu kabla ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho,” alisema Maganga.

Timu nyingine zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo ni pamoja na Don Bosco ya Congo, Zanaco ya Zambia pamoja na Vipers ya Uganda.  


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic