January 25, 2016

BOSSOU
Beki wa Yanga, Mtogo, Vincent Bossou, amesema tangu atue Bongo kucheza soka, hakuwahi kumuona straika hatari kwa kufunga mabao kama alivyo Mrundi, Amissi Tambwe.

Bossou ambaye amejiunga na Yanga msimu huu, tangu nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ awe majeruhi takriban miezi miwili sasa, amekuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara tofauti na hapo awali ambapo alikuwa akisugua benchi.

Bossou amesema kwa ushirikiano wa Tambwe na Donald Ngoma ni wazi wataifanikisha Yanga kuutetea ubingwa wao wa ligi msimu huu kutokana na kasi yao ya kufunga mabao ambapo Alhamisi iliyopita waliiwezesha timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji, huku Tambwe akifunga mabao matatu na kujichimbia kileleni kwa ufungaji akiwa na mabao 13.

“Kwa kweli sijawahi kuona mshambuliaji hatari zaidi ya Tambwe katika ligi hii kwani huyu jamaa anajua sana kufunga na huwa hana utani anapopata nafasi, naamini kwa kushirikiana na Ngoma (Donald) wataisaidia sana timu katika harakati zetu za kuwania ubingwa wa ligi,” alisema Bossou.


Ikumbukwe kuwa, mpaka mzunguko wa kwanza wa ligi unamalizika wiki iliyopita, Yanga imefunga mabao 36 huku 22 kati ya hayo yakiwa yamefungwa na Ngoma na Tambwe peke yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic