January 20, 2016


Mshambuliaji tegemeo wa Simba, Ibrahim Ajib, amelazimika kufanyiwa uchunguzi wa kina kutokana na jeraha la mbavu alilopata Jumamosi katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuparamiwa mgongoni na kiungo wa Mtibwa, Henry Joseph Shindika kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kulazimika kutolewa nje huku akimwaga machozi.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe, amesema kutokana na hali yake ilivyo, wamelazimika kumpeleka kwa doktari bingwa, Gilbert Kigadye wa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, ambaye ndiye pia hutibu wachezaji wa Yanga mara kadhaa, huku kwa sasa akiwa na kazi ya kuchunguza jeraha la nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyevunjika mfupa wa kisigino.

Gembe amewataka mashabiki wa Simba kuvuta subira kidogo kwani wanaweza kumkosa Ajib zaidi ya wiki kutokana na uchunguzi wa awali kuonyesha aliumia sana ubavuni.

“Ajib hatokuwepo kwenye mchezo wa kesho (leo, dhidi ya JKT Ruvu) kwa kuwa anatakiwa kupumzika kama wiki nzima ili kurejea kwenye mazoezi mepesi. Na kwa muda huo atakuwa chini ya uangalizi wa dokta, Gilbert,” alisema Gembe.


Wakati huohuo, winga Brian Majwega ambaye alisumbuliwa na jereha la goti anatarajia kuanza mazoezi muda wowote kuanzia leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic