Kocha Ahmed Morocco ameamua kuachana na ile ishu ya Ukurugenzi Mkuu wa Simba na kurudi zake kwao Zanzibar.
Hivi karibuni, Morocco alipewa jukumu la kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, akisaidiana na Boniface Mkwasa kama kocha mkuu kabla ya Simba kumfuata na kumpa kibarua cha kukinoa kikosi hicho.
Hiyo ni siku chache tangu ifahamike kuwa kocha huyo wa Mafunzo ya Zanzibar, huenda akasaini mkataba wa miezi sita wa kuwa mkurugenzi mkuu chini ya Mganda, Jackson Mayanja.
Morocco alisema kila kitu kilikwenda vizuri kuhusiana na kusaini mkataba kuanzia akiwa Unguja, Zanzibar, hadi alipofika jijini Dar es Salaam, lakini ghafla anashangaa rais wa Simba kubadilika.
“Hapa ninapoongea tayari nina nakala kutoka TFF inayoniruhusu kuifundisha Simba, nilikuwa nipo tayari kufanya nao kazi hata leo (jana), lakini makubaliano ya kimkataba tuliyokubaliana yamekuwa kinyume.
“Makubaliano tuliyokubaliana na Simba pamoja na TFF ni kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miezi minne na kama ingetokea nimepata majukumu ya kwenda kuitumikia timu ya taifa, basi ningefanya hivyo.
“Lakini cha ajabu na kushangaza leo (jana) asubuhi, rais wa Simba ghafla alibadilika katika hatua za mwisho kitu ambacho sijakitegemea kabisa, katika suala la mshahara ambao tulikuwa tumekubaliana tangu nilipokuwa Zanzibar limebadilishwa kwa kiwango kikubwa, sasa mimi nimeondoka nipo zangu Zanzibar, kama litatokeo lolote jipya nitarudi,”alisema Moroco.
0 COMMENTS:
Post a Comment