January 13, 2016

BOSSOU

Kikosi cha Yanga hivi karibuni kilitupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani hapa baada ya kufungwa na URA ya Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo inayofikia tamati leo.

Hali hiyo imesababisaha baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kutupwa nje ya kikosi hicho kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango cha juu katika michuano hiyo.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, ameliambia Championi Jumatano kuwa Yanga inapaswa kukifanyia mabadiliko makubwa kikosi chake kama inataka kufika mbali na kuachana na wachezaji ambao hawana faida klabuni hapo.

GABAR AKIKABIDHIWA JEZI YA YANGA

Alisema wachezaji kama Boubacar Garba na Vincent Bossou, hawana sifa ya kuitumikia Yanga, lakini pia hata katika kikosi chake hawawezi kupata nafasi ya kucheza.

Alisema kutokana na hali hiyo wachezaji hao wanapaswa kufungashiwa virago klabuni hapo kwa sababu wanachukua fedha za Wanayanga bure pasipo kufanya kazi ya maana uwanjani kama wanavyofanya wachezaji wenzao, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Amissi Tambwe.

"Ukiachana na wachezaji hao, vijana wengine kama Geoffrey Mwashuiya ambao bado wanahitaji kukomaa nao wanatakiwa kuondoka wakakomae kisoka na siyo kung'ang'ania kukaa benchi tu bila ya kucheza.

"Vinginevyo watazidi kusugua benchi na mwisho wa siku watafungashiwa virago wakiwa hawajafaidi lolote," alisema Maxime ambaye anasifika kwa kuibua na kukuza vipaji mbalimbali vya soka hapa nchini.

2 COMMENTS:

  1. Hicho ulichoongea ni kweli ila pia usisahau kuna Majadv,kiiza,kiongera na hata nimuboma hawana nafasi ya kuchezea Ndanda ya Mtwara!

    ReplyDelete
  2. Shombo tu ss mtibwa mnanini we mecky acha maneno y shombo fany kaz yko.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic