January 13, 2016


Beki tegemeo wa pembeni wa Azam FC, Shomari Kapombe, mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbagu na wenzao wawili wametengewa mazoezi maalum kutokana na majeraha ya enka.

Wakati wachezaji hao wakitengwa kwa ajili ya kufanya mazoezi hayo maalum, wengine wanaendelea na maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya African Sports itakayochezwa Jumapili hii.

Wachezaji wengine wenye majeraha hayo ya enka waliyotoka nayo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ni kinda, Abdallah Kheri na Mkenya, Allan Wanga, walioianza programu hiyo juzi Jumatatu asubuhi kwenye kambi za timu hiyo.

Programu hiyo inasimamiwa na kocha wa viungo wa timu hiyo, Adrian Dobre, ambaye amesema kuwa Kavumbagu ndiye pekee anahitaji mazoezi zaidi ili kumweka fiti.

Dobre alisema, nyota wengine waliobakia watarejea uwanjani kujumuika na wenzao ndani ya siku hizi mbili zijazo tayari kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu watakaocheza Jumamosi hii.

“Michuano ya Kombe la Mapinduzi imemalizika kwa kutolewa nusu fainali, lakini tumerejea na majeruhi wanne wenye majeraha ya enka ambao ni Kapombe, Kavumbagu, Abdallah na Wanga.

“Kati ya wachezaji hao Kavumbagu ndiye pekee anahitaji mazoezi zaidi ili kumweka fiti, lakini hao wengine wote ndani ya siku hizi mbili watarejea uwanjani tayari kwa ajili ya mechi ya ligi kuu,”alisema Dobre.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic