January 23, 2016


Katibu Mkuu Yanga, Dk Jonas Tiboroha ameambiwa kuchagua moja, kujiuzulu au afukuzwe kazi. Yeye ameamua kubwana manyanga na barua atakabidhi leo, rasmi.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza Dk Tiboroha ametakiwa kufanya hivyo baada ya kugundulika kulikuwa na madudu kibao wakati wa uongozi wake.

Imeelezwa, hiyo imetokana na kamati ya utendaji na uongozi wa juu wa Yanga kugundua kulikuwa na tatizo na mambo hayakwenda kama ilivyotakiwa kwa kufuata taratibu za kiungozi.

“Unajua Tiboroha ameharibu mambo mengi sana, lakini mwisho wake umekuwa ndiyo huo. Uongozi umekuwa mvumilivu sana na watu hawakujua tua.

“Lakini mwisho imegundulika kuna mambo kadhaa ambayo yalikiuka sababu za kiungozi na hayakuwa sawa. 


“Kamati ya utendaji pia imeridhia hilo baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kulibaini suala hilo,” kilieleza chanzo cha uhakika," kilieleza chanzo.

Lakini taarifa nyingine zinahusisha figisu ya masuala ya haki, unyoofu wa mambo katika masuala kadhaa na blogu hii inaendelea kufuatilia ili kupata uhakika kilichosababisha uongozi huo wa Yanga kufikia uamuzi huo na pia kuamua kumpa nafasi ya kujiuzulu mwenyewe au afukuzwe."

Juhudi za kumpata Dk Tiboroha katika simu kuanzia leo saa moja asubuhi hazikuzaa matunda kutokana na kuonekana simu yake ilikuwa imezimwa muda wote.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic