January 4, 2016


Simba imeanza michuano ya Mapinduzi kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walipanga kikosi cha wachezaji wengi ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza katika mechi za Ligi Kuu Bara na walionekana kutoelewana vizuri kabisa.

Pasi nyingi kwa Simba hazikuweza kuisaidia ingawa ilianza kupata bao la kwanza mapema tu kupitia kwa Awadhi Juma aliyelipa shuti kali nje ya 18, hiyo ilikuwa ni dakika ya 12.

Lakini Jamhuri wakasawazisha dakika chache baadaye kupitia kwa Mwalimu Mohammed katika dakika ya 18 aliyefunga kutokana na safu ya ulinzi ya Simba kuonekana kujichanganya huku Jonas Mkude na Mohammed Fakhi wakionekana kutoelewana.

Jamhuri ilipata bao la pili kupitia kwa Ammy Bangekesa  katika dakika ya 52 mara tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili lililotokana na makosa mengine ya Fakhi kabla ya Awadhi Juma kufunga bao la kusawazisha kwa Simba katika dakika ya 76.

Kutokana na wachezaji wengi wa Simba kuboronga, Kocha Dylan Kerr aliamuwa kuwaingiza Hamisi Kiiza, Dani Lyanga, Ibrahim Ajib na Mwinyi Kazimoto ambao waliiwezesha Simba kutawala mchezo zaidi.


1 COMMENTS:

  1. Kuna wakati nashindwa kuelewa anachokitafuta kocha wa Simba. Mpaka sasa huyu jamaa Jana First Eleven. Haya Mambo yaliwashinda Liverpool. Huwezi kwenda mashindanoni kufanya majaribio.

    Angetumia fulsa hii kuendelea kuwapanga wachezaji watakaoendelea kuelewana pindi wanapokuwa uwanjani. Simba haichezi sasa kama timu kubwa, wachezaji hawaelewani, huoni wakiji- position uwanjani kama Professional players, unamwangalia Kiongera unajiuliza sababu ya Simba kumuacha Maguli unapata kichefuchefu.

    Wachezaji wengi walioachwa Simba ni wazuri kuliko waliosajiliwa. Tena wanafanya vizuri katika club zao.

    Simba imefungwa goli la pili takribani dk ya 52 halafu mtazame kocha anaetaka kupata matokeo anafanya sub ya maana dakika ya ngapi.

    Inaboa sana kuitazama Simba sasa ikiwa inacheza, hakuna haja ya kuwa na kocha na kukaa kambini kwani hatuoni mpira wa kufundishwa.

    Tazizo la beki wa kati lilijulikana na Dirisha dogo lilikuwepo ila ona walichofanya kocha pamoja na uongozi. Seriously kuna wachezaji wamesajiliwa Simba na hawana hadhi ya kucheza Simba au hawajitambui kabisa.

    Am out

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic