January 13, 2016


Mtibwa Sugar imezidi “kutokuwa na bahati” na fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kulikosa kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Mwaka jana iliingia fainali dhidi ya Simba, ikapoteza lakini leo imepoteza tena kwa kuchapwa mabao 3-1 na URA ya Uganda katika mechi iliyoisha hivi punde kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Bao la kwanza lililofungwa na Julius Ntambi kwa kichwa, lilidumu hadi mwisho wa dakika 45 na timu ziliporejea uwanjani ilionekana kama Mtibwa Sugar wamejiandaa kusawazisha.


Hata hivyo, mambo hayakuwa mazuri baada ya kufungwa mabao mengine harakaharaka yakifungwa na David Lwasa aliyeingia kipindi cha pili ambaye alitumia makosa mara mbili ya mabeki wa Mtibwa Sugar ambao mwishoni walionekana kuchoka.

Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 90 na Jaffar Salum baada ya kipa wa URA kufanya mzaha na mfungaji akampokonya mpira na kuutupia wavuni.

Mtibwa Sugar imecheza fainali tano na kubeba kombe la Mapinduzi mara moja tu, huku ikipoteza mara nne.

Bingwa wa michuano hiyo URA ameondoka na Sh milioni 10, huku washindi wa pili Mtibwa Sugar wakilamba Sh milioni 5.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic