URA inakwenda fainali baada ya kung'oa Yanga kwa penalti 4-3
YANGA: Wamepata penalti 3
Kelvin Yondani PATA
Geofrey Mwashiuya KOSA
Malimi Busungu KOSA
Simon Msuva PATA
Deo Munish PATA
URA: Wamepata penalti 4
Jimmy Kulaba PATA
Simon Sekito KOSA
Sidi Kieune PATA
Deo Otieno PATA
Brian Bwete PATA
MPIRA UMEKWISHAAAA
Dk 90+2 inapigwa kona nyingine, hatari Lwasa anapiga lakini inakuwa goal kick
Dk 90+1 Juma Abdul anafanya kazi ya ziada na kutoa mpira inakuwa kona, inachongwa hatari lakini Dida anaokoa.
+3
Dk 87 hadi 90, URA wanaonekana kuridhika na sare kwa kuwa zaidi wanapoteza muda
SUB Dk 87, Paul Nonga anaingia kuchukua nafasi ya Tambwe
SUB Dk 84 Deogratius Otieno anaingia kuchukua nafasi ya Julis Ntambi upande wa URA
SUB Dk 79, Salum Telela anaingia kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite
GOOOOOOO Dk 76 Peter Lwasa anaifungia URA bao la kusawazisha baada ya kupiga pasi zaidi ya 10
SUB Dk 75, Yanga wanamtoa Ngoma na nafasi yake anachukua Malimi Busungu
SUB Dk 70 Geofrey Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke
Dk 67,Ngoma anaingia vizuri lakini anaangushwa. Mwamuzi anasema hakuguswa, twende.
SUB Dk 62 URA wanamtoa mkongwe Masaba na nafasi yake inachukuliwa na Peter Lwassa
Dk 59, Msuva katika nafasi nzuri lakini anashindwa kufunga baada ya kuwa amepoteza balance
Dk 55, Deus Kaseke anatoa pasi nzuri kwa Tambwe anauwahi mpira na kupiga, lakini unatoka sentimeta chache kabisa nje ya lango la URA
Dk 52 Juma Abdul anapiga mpira safi wa adhabu, Tambwe anajitwisha lakini inakuwa goal kick
Dk 47 hadi 50, URA wanaonekana kupanga mipango mingi na Yanga hawajarejea tena kwenye lango la Waganda hao
Dk 46, Yanga wanafanya shambulizi, Msuva anapiga shuti kali lakini linagonga nyavu za pembeni
MAPUMZIKO
Dk 42 hadi 45, bado mpira zaidi unachezwa katikati zaidi.
Dk 40 hadi 44, mpira zaidi unachezwa katikati, URA wanaonekana kujipanga vizuri lakini bado wanashindwa kuwa na mipango mizuri ya mwisho
Dk 49, Tambwe anaingia vizuri ndani ya eneo la hatari lakini anagongana na kipa. Anatolewa kwenda kutibiwa
Dk 34 Mkumbwa tena anapiga shuti baada ya kugongena vizuri na Samwel lakini anashindwa kulenga
Dk 27 hadi 29, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali.
Dk 25 Elikana Mkumbwa anaingia katika eneo la hatari la Yanga lakini Yondani anawahi kuondoa
Dk 20 Samuel anafanya kazi ya zida kuokoa krosi ya Msuva na kuwa kona lakini haina matunda
Dk 17, Elikana Mkumbwa anamgeuza Juma Abdul na kupiga shuti kali lakini linatoka nje kidogo
DK 15, krosi nzuri ya Masaba lakini inaokolewa na kamusoko
GOOOOOO Dk 13, Amissi Tambwe anafunga bao safi la kichwa kwa kuunganisha krosi nzuri ya Msuva. Ni bao lake la kwanza la michuano ya Mapinduzi
Dk 9, krosi safi kabisa ya Msuva inamfikia Ngoma lakini anashindwa kuitumia kwa kupiga shuti na kupaisha
Dk 3 Yanga wanakuwa wa kwanza kufanya shambulizi lakini Kamusoko anashindwa kumalizia.
0 COMMENTS:
Post a Comment