URA ya Uganda imewang’oa Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, leo.
Wakati wengi walitarajia fainali itakuwa Simba dhidi ya Yanga, lakini timu zote zimeshindwa kufika fainali baada ya Mtibwa Sugar kuing’oa Simba katika mechi ya jioni na Yanga ikaondolewa na Waganda hao kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
URA imeitoa Yanga kwa mikwaju 4-3 ya penalti baada ya timu hizo kwenda sare ya 1-1 katika dakika 90.
Yanga walipata bao kupitia Amissi Tambwe katika dakika ya 13 aliyefunga kwa kichwa, URA wakasawazisha kupitia David Lwasa katika dakika ya 83 baada ya kuutegua mtego wa kuotea wa mabeki wa Yanga uliongozwa na Vicent Bossou.
Wakati wa mikwaju ya penalti, Geofrey Mwashiuya na Malimi Busungu walikosa upande wa Yanga wakati Simon Sekito alikosa upande wa URA.
YANGA: Wamepata penalti 3
Kelvin Yondani PATA
Geofrey Mwashiuya KOSA
Malimi Busungu KOSA
Simon Msuva PATA
Deo Munish PATA
URA: Wamepata penalti 4
Jimmy Kulaba PATA
Simon Sekito KOSA
Sidi Kieune PATA
Deo Otieno PATA
Brian Bwete PATA
0 COMMENTS:
Post a Comment