January 20, 2016




Dk 87 hadi 90 Simba wanaonekana kugongeana pasi fupi wakionyesha kupoteza muda na kuridhika na bao mbili.
Dk 86 Simba wanafanya shambulizi  kali sana, Kiiza anapiga kipa Hamisi anaokoa, Kazimoto anapiga shuti kali beki JKT anaokoa kwenye msitari, Kiongera anaupoteza mpira huo.

SUB 82 Kazimoto anaonyeshwa kadi ya njano halafu anajiangusha
Dk SUB Dk 81 Saad Kipanga anaingia kuchukua nafasi ya Kamuntu upande wa JKT
Dk 80, Agbani anadaka mpira na kuonyesha mbwembwe za danadana akilenga kupoteza muda

Dk 78, Juuko anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliokuwa unamfikia Kamuntu, inakuwa kona na Michael Aidan anachonga mpira, unatoka...goal kick
Dk 78, Kiiza anapiga kichwa safi, lakini kipa Hamisi Seif wa JKT anadaka vizuri kabisa

Dk 73, Kiongera anapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya Kiiza kumpa pasi nzuri
KADI Dk 69 anatoka Lyanga upande wa Simba anaingia Rafael Kiongera
SUB Dk 66 JKT inamtoa Hamis Thabit anaingia Najim Magulu
Dk 64, Lyanga anamtoka beki wa JKT anabaki yeye na kipa lakini anashindwa kufunga
GOOOOO Dk 62, pasi ya kipa Vicent Agbani inamfikia Lyanga, anampiga chenga kipa wa JKT na kufunga bao la pili
KADI Dk 59 Nashon Nathan na Kessy, kila mmoja analambwa kadi ya njano
GOOOOOOO Dk 54 Kiiiiza anafunga vizuri penalti na kuiandikia Simba bao la kwanza

PENAAAAAT Dk 51 Mwamuzi Martin Saanya anasema ni penalti baada ya Lyanga kuangushaKADI Dk 50 Juuko anamtandika Kamuntu na kulambwa kadi ya njano
Dk 48, Kessy anawapiga chenga mabeki wawili wa JKT lakini anashindwa kufikia lengo, wanaokoa

Dk 47 Kamuntu anapiga kichwa safi lakini anashindwa kulenga
SUB DK 46 Simba wanamtoa Mwalyanzi, nafasi yake inachukuliwa na Hassan KessyMAPUMZIKO
SUB Dk 45, Simba wanamuingiza Abdi Banda kuchukua nafasi ya Tshabalala aliyeumia
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA (+3)
Dk 43, krosi nzuri ya Nimubona, Kiiza anaukosa mpira JKT wanaokoa safi kabisa
KADI Dk 41, Kamuntu analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Tshabalala
Dk 38 krosi nzuri ya Tshabalala lakini kipa wa JKT anaibuka na kudaka vizuri
Dk 32 hadi 35 mpira unaonekana kupooza, Simba wanaounguza kasi na JKT taratibu wanabadilika na kuongeza kumiliki mpira

DK 31, Aidan anapiga shuti kali kwa kushitukiza,  lakini anashindwa kulenga lango
Dk 25, kipa JKT anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguu mwa Kazimoto. Anaumia na sasa anatibiwa
Dk 23, Lyanga anapiga krosi safi kabisa, kipa anaokoa mpira unamkuta Nimubona anapiga shuti kuubwaaaaaa nje..

Dk 13 hadi 17, inaonekana hakuna shambulizi kali upande wowote, zaidi mpira unachezwa pasi nyingi katikati ya uwanja
Dk 11, Kamuntu anapiga krosi, Isihaka anaokoa nakuwa kona. Inachongwa na Michael Idan lakini Simba wnaokoa
Dk 8 na 10, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja, angalau JKT wanaonekana lakini Simba wanatawala zaidi
Dk 7 Isihaka analazimika kumrudishia kipa wake baada ya kupata presha ya Kamuntu

Dk 5, Nimubona anachonga krosi, JKT wanaokoa na kuwa kona ya kwanza ya mchezo, inachongwa na Nimubona lakini kipa anawahi na kuokoa Dk 3, Issa Said wa JKT anapiga krosi ndefu lakini mpira unaishia mikononi mwa Agbani
Dk 2 Emiry Nimubona anaingia vizuri na kupiga krosi, Kiiza anajaribu kugeuka lakini mpira unaokolewa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic