Hii ndiyo habari ya mjini pale mjini Shinyanga, kwmaba straika Elias Maguri wa Stand United hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu yake jambo linalompa ugumu kupambana na Amissi Tambwe wa Yanga kuwania ufungaji bora.
Katika Ligi Kuu Bara hadi sasa, Tambwe anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 13, akifuatiwa na Hamis Kiiza wa Simba mwenye mabao 10 huku Maguri akiwa na mabao tisa sawa na Donald Ngoma wa Yanga.
Maguri amepoteza nafasi kikosi cha kwanza baada ya kuvurugana na kocha wake, Patrick Liewig siku chache baada ya kung’ara na kikosi cha Taifa Stars na Kilimanjaro Stars.
Taifa Stars ilipocheza dhidi ya Algeria mwaka jana kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018, Maguri aliifungia Stars bao moja katika sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.
Maguri alisema; “Sina nafasi kikosi cha kwanza, hivyo siwezi tena kuwania tuzo ya mfungaji bora na nawaachia vita hiyo, Tambwe na Kiiza.
“Kocha hataki kunipanga kwa sababu eti mimi ni staa na yeye hataki mchezaji staa katika kikosi chake jambo ambalo siyo kweli, Tambwe na Kiiza wao wana nafasi katika vikosi vyao, hivyo wanaweza kufanya vizuri.”
Alipotafutwa Liewig, alisema; “Mtu hajitumi nimpe nafasi ili iweje? Tangu aliporudi amekuwa wa kawaida mno kikosini.”
0 COMMENTS:
Post a Comment