January 23, 2016


Kazi ipo Uwanja wa Taifa kesho Jumapili wakati Yanga itakapoivaa Friends Rangers katika michuano ya Azam Sports au Kombe la FA.

Friends Rangers timu ya Ligi Daraja la Kwanza, imepanga kuwatumia mastraika wake hatari ambao wamewahi kucheza katika klabu za Sweden na Dubai ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.

Kocha wa Friends Rangers, Herry Mzozo, alisema atamtumia straika, Juma Mgaya ambaye amewahi kucheza nchini Sweden na Cosmas Lewis ‘Balotelli’ aliyewahi kucheza Dubai.

 “Hao Yanga ni timu kongwe tu na siyo timu ya kututisha sisi, tuna mikakati yetu ya kuhakikisha tunashinda, ndiyo maana tunao hao wachezaji,” alisema Mzozo. 

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema: “Tumejiandaa vizuri kwa mechi hii, labda niseme wazi tu kwamba tutatumia kikosi cha pili kwa lengo la kupumzisha wachezaji wetu.”

Katika michuano hiyo, leo Jumamosi Simba itacheza na Burkina Faso kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati jijini Mwanza, Pamba itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


Mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Ndanda FC itacheza na Mshikamano FC. Mechi nyingine za kesho Jumapili, Njombe Mji itacheza na Prisons kwenye Uwanja wa Amani, Njombe na Stand United itaivaa Mwadui FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic