January 15, 2016

RAIS wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amefunguka juu ya ujio wa Kocha Kim Poulsen ambaye yuko jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na taarifa ujio wake umetokana na kuitwa na TFF.

Malinzi amesema kuwa kocha huyo ambaye ni wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, yupo nchini kwa ajili ya mapumziko binafsi akiwa na familia yake na kilichotokea ni kuwa alikutana naye na kula naye chakula cha mchana.

Akizungumzia suala hilo, Malinzi alinukuliwa akisema: “Kim alikuja akiwa na familia yake kwa ajili ya mapumziko, nilionana naye na kula naye chakula cha mchana pamoja.”

Alipotakiwa kufafanua juu ya kuwa kuna uwezekano akapewa ajira yoyote chini ya utawala wake, Malinzi alisema: “Siwezi kulizungumzia hilo kwa sasa.”

Kim raia wa Denmark aliondolewa kwenye nafasi ya ubosi wa Stars na uongozi wa Malinzi ulipoingia madarakani, hakupatikana kuzungumzia juu ya ujio wake huo.

Juzi picha ya Malinzi na Kim ilisambazwa ikiwaonyesha wapo katika hoteli moja karibu kabisa Mbuyuni jijini Dar es Salaam.

Taarifa za ndani kutoka TFF zinaeleza mazungumzo hayo ni kumpa nafasi ya kuzinoa timu za vijana ili kutimiza malengo ya kufanya vizuri Kombe la Dunia na Olimpiki kama ambavyo TFF imejiwekea malengo ya 2020.

TFF wamekuwa wakifanya siri kulizungumzia suala hilo linalomhusu Kim ambaye kuondolewa kwake na kuajiliwa Mart Nooij kulizua mjadala mkubwa kwa kuwa ni kocha aliyechangia vijana wengi kukua.

Kim alitoa nafasi kubwa kwa vijana kuichezea Taifa Stars akianza na akina Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva, Frank Domayo na wengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic