January 15, 2016



Kocha Kim Poulsen yuko jijini Dar es Salaam na taarifa zinasema kwamba ametua nchini kwa ajili ya kuzungumza na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Tayari Kim raia wa Denmark aliyewahi kuwa kocha wa taifa Stars kabla ya kuondolewa na uongozi mpya wa Jamal Malinzi ulipoingia madarakani, ameanza mazungumzo na TFF.

Picha yake akiwa na Malinzi, katika hoteli moja karibu kabisa Mbuyuni jijini Dar es Salaam, imekuwa gumzo mitandaoni.

Taarifa za ndani kutoka TFF zinaeleza mazungumzo hayo ni kumpa nafasi ya kuzinoa timu za vijana ili kutimiza malengo ya kufanya vizuri Kombe la Dunia na Olimpiki kama ambavyo TFF imejiwekea malengo ya 2020.

TFF wamekuwa wakifanya siri kulizungumzia suala hilo linalomhusu Kim ambaye kuondolewa kwake na kuajiliwa Mart Nooij kulizua mjadala mkubwa kwa kuwa ni kocha aliyechangia vijana wengi kukua.

Kim alitoa nafasi kubwa kwa vijana kuichezea Taifa Stars akianza na akina Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva, Frank Domayo na wengine.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic